CCM Yashinda Viti Vyote Udiwani Sengerema, Tarime Mjini | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 29, 2020

CCM Yashinda Viti Vyote Udiwani Sengerema, Tarime Mjini

  Malunde       Thursday, October 29, 2020


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti vyote 47 vya udiwani katika majimbo ya Sengerema na Buchosa wilayani Sengerema.

Pia, chama hicho kimeshinda uchaguzi katika kata zote nane za jimbo la Tarime Mjini katika uchaguzi uliofanyika jana.

Wakati msimamizi wa uchaguzi jimbo la Sengerema, Magesa Mafuru akisema CCM imeshinda kata zote 26 za jimbo hilo, mwenzake Crispin Luanda wa Buchosa amesema chama hicho kimetwaa kata zote 21 za halmashauri hiyo.

Wakizungunza kwa nyakati tofauti leo Oktoba 29, 2020, wasimamizi hao wamesema shughuli ya majumuisho ya kura za ubunge na urais katika majimbo hayo inaendelea.

Kwa upande wa jimbo la Tarime Mjini, msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Elias Ntiruhungwa amesema kuwa awali wagombea udiwani katika kata mbili katika jimbo hilo wapita bila kupingwa.

Amesema kuwa katika kura zilizopigwa jana kata zilizobaki sita CCM imeweza kushinda huku akisema kuwa matokeo ya ubunge yanatarajiwa kutangazwa muda wowote.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post