NEC YAWAONYA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI MKOA WA SINGIDA

NEC YAWAONYA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI MKOA WA SINGIDA



Mkurugenzi wa Manunuzi na Lojistik wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Emmanuel Urembo akihutubia wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoa wa Singida uliofanyika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa mkoani hapa.


Afisa Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Amos Madaha (kulia), akizungumza katika mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoa wa Singida uliofanyika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa mkoani hapa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Singida, Evodius Katare na kulia ni Mkurugenzi wa Manunuzi na Lojistik wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Emmanuel Urembo.

Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Singida, Evodius Katare, akizungumza kwenye mkutano huo.

Wadau wa uchaguzi wakishiriki katika mkutano huo.

Wadau wa uchaguzi wakishiriki katika mkutano huo.

Mmoja wa kiongozi wa dini ya Kiislamu Hamisi Kisuke, akishiriki mjadala kwenye mkutano huo.


Askofu Jonas Kaaya wa Kanisa la KLPT, akishiriki mjadala. 

Mchungaji Dkt. Syprian Hilinti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ((KKKT) Singida akishiriki mjadala kwenye mkutano huo.

Zainabu Ally kutoka Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Singida, akiuliza swali.

Wadau wa uchaguzi wakishiriki katika mkutano huo.

Mdau wa uchaguzi Boniface Kitiku, akiuliza swali kwenye mkutano huo.


Mdau kutoka makundi ya wanawake, Happy Francis akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Mdau wa uchaguzi, Pascal Ntatau akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Kiongozi wa Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) Mkoa wa Singida, Ndugu Samwel akichangia mjadala kwenye mkutano huo.


Msaidizi wa Kisheria kutoka Shirika la SIPACE, Fatuma Abeid  akichangia jambo.




Na Dotto Mwaibale, Singida.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa tahadhari kwa Vyama vya siasa wagombea nafasi mbalimbali za uongozi na wananchi kuwa wajihadhari na vitendo ama matamshi ambayo yanaweza sababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi kuwa watachukuliwa hatua kwani sheria za nchi hazijasimama.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manunuzi na Lojistik wa tume hiyo, Emmanuel Urembo wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoa wa Singida uliofanyika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa mkoani hapa.

"Wakati Tume inaendelea kuratibu kusimamia na kuendesha uchaguzi huu kwa kutumia sheria za uchaguzi, Vyama vya siasa wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi hiki, sheria nyingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo ama matamshi ambayo yanaweza sababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi." alisema Urembo.

Alisema Tume inawahakikishia wananchi kuwa imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata Katiba, Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali na inaamini kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu Watanzania wataweza kupiga kura kwa amani siku ya uchaguzi.

Urembo alisema Tume inatumia nafasi hii pia kuwatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalumu kwa kuwa maelekezo yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu, wajawazito, akina mama wanaonyonyesha watakaokwenda na watoto vituoni, wazee na wagonjwa.

Aliongeza kuwa kwa wale wasiojua kusoma na kuandika wataruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

" Kwa watu wenye ulemavu wa kuona kila kituo cha kupigia kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu 'tactile ballot folder' hii ni kwa wale wanaofahamu kutumia maandishi hayo na wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemuamini wa kuweza kumsaidia." alisema Urembo.

Aidha Urembo alisema kwa wenye ulemavu wa viungo vituturi vitakavyotumika kupiga kura vinaruhusu kuwahudumia kwani kuna pande mbili tofauti, upande mmoja kuna urefu wa kutosha na kikigeuzwa kinakuwa kifupi kumwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.

Urembo alitumia fursa hiyo kuwaambia kuwa kila mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze na kadi yake ya kupigia kura katika kituo alichojiandikisha ili kutimiza haki yake ya msingi ya kikatiba na kuwa Tume itaendelea kutoa taarifa kwa wakati na kwa njia mbalimbali kuhakikisha wananchi wanafahamu na kuelewa mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527