WAGOMBEA MULEBA KUSINI WAJINOA VIKALI


Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Muleba Kusini Dr. Oscar Kikoyo baada ya kupokea Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Costancia Buhiye na kuahidi kuinadi kwa wananchi.
 ***
Na Ashura Jumapili,Muleba
Wagombea wa Jimbo la Muleba Kusini mkoani Kagera katika nafasi ya Ubunge na Madiwani wameanza kunoa makali kupitia mikutano tofauti ya awali kabla ya uzinduzi rasmi wa kampeni utakaofanyika kesho siku ya Jumamosi Septemba 6,2020.

Mgombea Ubunge Jimbo la Muleba kupitia CCM Dr.  Oscar Kikoyo kwa nyakati tofauti ameshiriki mikutano iliyomkutanisha na wagombea wengine wa Ubunge na Udiwani kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanyika katika uwanja wa Zimbihire mjini Muleba kesho Jumamosi.

Dr. Kikoyo ameahidi kuinadi Ilani ya uchaguzi ya CCM (2020-2025) inayotoa mwelekeo wa ongezeko la miradi ya maendeleo na kutoa ufumbuzi wa changamoto zilizobaki katika awamu ya kwanza ya uongozi wa miaka mitano wa Rais John Magufuli.

Akiwa katika Kata ya Nshamba  Dr. Kikoyo ameahidi kushirkiana na diwani wa Kata hiyo na wadau wengine kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la uhaba wa maji na kuinua elimu hasa ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita katka Jimbo la Muleba.

Mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM mbali na kukutanisha pamoja wanachama wa CCM viongozi na wananchi pia unatarajiwa kupambwa na wasanii kutoka ndani na nje ya Wilaya ya Muleba ambapo wagombea udiwani wote wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.
Mgombea Ubunge wa Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo akihutubia wananchi wa Kata ya Nshamba eneo la Muzinga na kuwaahidi kasi ya maendeleo.
Baadhi ya wanachama na mashabiki wa CCM katika mkutano wa kampeni Kata ya Nshamba Jimbo la Muleba Kusini.
Mgombea Udiwani Kata ya Nshamba Gosbert Masilingi akijinadi kwa wananchi wa Kata hiyo kuomba achaguliwe tena kutekeleza ilani ya chama chake.
Mgombea Udiwani kata ya Kibanga Edson Issaya akinadi ilani ya CCM na mgombea wa chama hicho katika Kata ya Nshamba Gosbert Masilingi.
Mgombea Ubunge Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo akijadili jambo na baadhi ya wananchi baada ya mkutano katika eneo la Muzinga Kata ya Nshamba.
Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Kagera Wilbroad Mutabuzi akitoa nasaha kwa wagombea waliopita kwenye uteuzi wa vikao vya chama kunadi mafanikio ya awamu iliyopita na ilani ya Uchaguzi ya CCM
Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Mazinga iliyoko kwenye Ziwa Victoria Edson Alex akiwa tayari kusaka kura zake na wagombea wengine baada ya kukabidhiwa ilani na vitendea kazi vingine.
Mgombea udiwani kata ya Kishanda Helmes Mushumbusi akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika Kata ya Nshamba

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post