Tanzia : MWANAMUZIKI SAID MABELA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA

 Gwiji wa ukung’utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabela amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.


Mabela ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.

Mtoto wa marehemu, Mabela Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post