Picha : MVUA YA UPEPO YAANGUSHA MNARA WA MATANGAZO RADIO FARAJA NA KUPONDA KANISA LA MAMA MWENYE HURUMA NGOKOLO

Muonekano wa  mnara wa kurushia matangazo Redio Faraja Fm Stereo ukiwa umeangukia paa la Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha jana Jumatatu Septemba 28,2020. 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mnara wa Kurushia Matangazo wa Kituo cha Redio Faraja Fm Stereo umeanguka kisha kuponda Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga na kusababisha uharibifu wa mali kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha jana Jumatatu Septemba 28, 2020 kuanzia saa 12 jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Jimbo la Shinyanga, Padre Anatoly Salawa amesema mvua iliyoambatana na upepo iliyonyesha jana jioni imeleta madhara katika Kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo sambamba na upande wa Radio Faraja na Radio Kwizera ambayo pia inatumia mnara huo kurusha matangazo yake Mjini Shinyanga.

“Mnara wetu wa Matangazo wa Radio Faraja wenye urefu mita 60 kwenda juu umeanguka na kuvunja paa la Kanisa upande wa nyuma. Tunashukuru kutokana na uimara wa kanisa hakuna madhara makubwa sana yaliyotokea na wakati tukio linatokea hapakuwa na watu kanisani”,amesema Padre Salawa.

“Tangu madhara yatokee hatupo hewani,Mpaka sasa tumezima matangazo na tutarejesha mara baada ya kupokea mitambo kutoka Mgodi wa Mwadui kwa ajili ya kuondoa mnara ulioanguka na tutarejesha matangazo tukitumia sehemu ya mnara wa msalaba/kengere uliobakia lakini kule Kahama na kwenye mitandao ya kijamii tunaendelea na matangazo yetu”,ameeleza Padre Salawa.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Idara ya Mawasiliano Jimbo la Shinyanga amesema tayari viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga wakiongozwa na Askofu Liberatus Sangu ambapo amewaomba waumini na wadau mbalimbali kuchangia ukarabati wa Kanisa ili lirudi kwenye hali ya kawaida.

Padre Salawa amewaomba wadau wa Redio na Kanisa,Waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuguswa na kutoa michango mbalimbali ili hatua za kufanya ukarabati wa kanisa na mitambo ya Redio iliyoathiriwa ziweze kuanza mara moja.

"Michango yote iwekwe kwenye Akaunti maalum ya jimbo la Shinyanga Benki ya CRDB yenye namba 01J1058390001 DIOCESE OF SHINYANGA na kwa njia ya M-PESA kwa namba 0762444746 yenye jina la Liberatus Sangu",amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba kutokana na mvua iliyonyesha jana ambayo iliambatana na upepo mkali imesababisha uharibifu wa mali katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ikiwemo kuangusha mnara wa kurushia matangazo ya Radio Faraja Fm na kupelekea paa la kanisa kuanguka na mabati kadhaa kuharibika. 

Amesema pia mvua hiyo ilisababisha kuanguka kwa mnara wa mawasiliano uliopo kituo Kikuu cha Polisi wilaya ya Shinyanga na kupelekea uharibifu wa gari namba lenye namba za usajili T.234 BJK aina ya Noah ambayo ni kielelezo cha Traffic kesi. 

Amesema zoezi kupata thamani halisi ya mali zote zilizoharibiwa linaendelea kufanyika.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Jimbo la Shinyanga, Padre Anatoly Salawa akielezea kuhusu madhara yaliyojitokeza baada ya Mnara wa Matangazo ya Redio Faraja kuangukia Kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo kufuatia mvua kubwa iliyoambata na upepo kunyesha jana jioni Septemba 28,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Jimbo la Shinyanga, Padre Anatoly Salawa akionesha Mnara wa Matangazo ya Redio Faraja ulioangukia Kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo.
Muonekano wa  mnara wa kurushia matangazo Redio Faraja Fm Stereo ukiwa umeangukia paa la Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga 

Muonekano wa  sehemu ya ndani ya Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga baada ya kuangukiwa na Mnara wa Matangazo ya Radio Faraja Fm Stereo 

Muonekano wa  mnara wa kurushia matangazo Redio Faraja Fm Stereo ukiwa umeangukia paa la Kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527