Picha : TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WATOA HUDUMA YA HABARI MITANDAONI 'BLOGGERS'... 'YASISITIZA UMAKINI MTANDAONI'



Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.

****

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ‘Online Content Service Providers’ nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 28,2020.

Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Septemba 15,2020 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .

Akifungua Mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles amesema Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ni wadau muhimu katika mchakato wa uchaguzi ndiyo maana wameamua kukutana nao ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uchaguzi ili waweze kuandika habari kwa usahihi na kulinda amani ya nchi.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi tunavipongeza vyombo vya habari mtandaoni kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkitupatia.Tunathamini mchango wenu na tutaendelea kushirikiana nanyi ili kujenga nchi yetu. Tumewaita ili kuwajengea uelewa kuhusu mkachato wa uchaguzi,tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu taratibu mbalimbali za uchaguzi”,amesema Dkt. Charles.

Aidha amewataka waandishi wa habari kuvipa nafasi sawa vyama vyote vya siasa na kuepuka kuandika habari zenye kuhamasisha vurugu na kusababisha uvunjivu wa amani.

“Kipindi cha Kampeni za uchaguzi huwa kuna joto la uchaguzi ambapo joto la kuvunja amani nalo huongezeka. Naomba tulinde amani ya nchi yetu kwa kuepuka kuandika habari zenye kuleta chuki”,amesema.

Katika hatua nyingine alivitaka vyama vya siasa kufuata maadili ya uchaguzi na sheria za nchi na kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu huku akivikumbusha vyombo vya habari kuepuka kuandika kauli na matamshi ya kuvunja amani.

“Kuanzia sasa tutachukua hatua kali kwa viongozi wanaotoa matamshi ya kuvunja amani. Hata wewe mwandishi wa habari ukiandika habari zenye kuunga mkono matamshi hayo nawe utakuwa unavunja amani”,ameongeza Dkt. Charles.

Dkt. Charles ametumia fursa hiyo kuviomba vyombo vya habari kuelimisha jamii kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura Oktoba 28,2020 ili kupata viongozi wanaowataka watakaowaletea maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari, amesema.

"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi”.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati wa Mkutano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),uliofanyika leo katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpigakura, Giveness Aswile akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati wa Mkutano huo kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi”, alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari.


Baaadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri

Kushoto ni Mkurugenzi wa Kahama Tv Online, Shija Felician na Mkurugenzi wa Malunde Media, Kadama Malunde wakiwa kwenye Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni

Sehemu ye Meza kuu 
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527