MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI (CCM) DKT. TULIA ACKSON AZIDI KULITIKISA JIJI LA MBEYA


September 15, 2020 Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dkt. Tulia Ackson akiwa kwenye kampeni katika kata ya igawilo iliyopo jijini humo ambao amewaeleza Wananchi baadhi ya mambo ambayo Serikali imeyabainisha katika Ilani yake endapo wataichagua katika uchaguzi mkuu wa October 28, 2020

“Ndugu zangu wa Mbeya siku zote nimekuwa nikiwaeleza kwamba CCM inahoja na wale wenzetu wanavihoja, tumejipanga kutatua changamoto mbalimbali hapa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara ya njia nne, kumaliza tatizo la maji na umeme, ajira kwa vijana na wakinamama”

“Kuna watu wanasema kwamba eti muogopeni Tulia kama Corona, nimewaambia hao jamaa kwamba mwaka huu hatudanganyiki na ndio maana hata katika kipindi cha Corona yenyewe hao hao watu walikimbia Bungeni. Sasa waambieni hatuwezi kumuogopa Tulia kwasababu hata hiyo Corona yenyewe haipo…”-Dr. Tulia Ackson

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post