Picha : NHIF WAZINDUA VIFURUSHI BIMA YA AFYA KWA WAANDISHI HABARI


Na Marco Maduhu - Mwanza.
Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF imezindua rasmi vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi habari, ili kuwarahisishia kupata matibabu kipindi watakapougua na kuokoa maisha yao.


Zoezi hilo limefanyika leo kwenye Ofisi za NHIF Jijini Mwanza, na kuhudhuriwa na wadau wa habari akiwamo Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandis Francis Mihayo, na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi Anjelina Mabula ,huku Mgeni Rasmi akiwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa bBima ya Afya Bernard Konga, amesema waandishi wa habari ni kundi muhimu sana katika upataji wa bima hiyo ya afya, ambapo wengi wao hawana ajira rasmi, hivyo itawasaidia kupata matibabu kwa urahisi na kutotumia gharama kubwa.

Amesema awali waandishi wa habari walikuwa wakijipenyeza kujiunga vifurushi vya bima hiyo ya afya kwenye makundi mengine wakiwamo bodaboda, ambapo walikuwa wakiondolewa kwa sababu hawakuwa wahusika.

"Tulikaa na viongozi wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC, tukalizungumza hili suala la kuanzisha vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari na kufikia makubaliano ambapo leo zoezi hili tumelizindua rasmi," amesema Konga.

"Gharama za Mwandishi wa habari kukata Kadi ya bima ya afya kwa mwaka mmoja ni Shilingi 100,000 pamoja na wategemezi wao kiasi hicho hicho cha pesa," ameongeza.

Aidha amewataka waandishi wa habari kuchangamkia fursa hiyo, ikiwa kwa sasa bado wanasuasua, ambapo kati ya waandishi wa habari 1,800 waliopo kwenye Press Clubs waliokata bima hiyo wapo 65 na wategemezi wao 20.

Pia ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania wakate bima hiyo ya afya ili kuwasaidia kupata matibabu bure pale watakapopatwa na maradhi ghafla, na kubainisha Kati ya Watanzania Milioni 60 walio na kadi hizo ni Milioni 4.4.

Naye mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mfuko huo wa bima ya afya umefanya kitu cha muhimu sana kwa kukumbuka mhimili huo wa Nne usio rasmi kwa kujali afya zao.

Amesema hakuna kitu cha muhimu sana katika maisha ya binadamu kama mtaji wa afya, ambapo bila afya shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika, na kutoa wito kwa waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla wakate bima hiyo ya afya.

Kwa upande wake Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Deogratius Nsokolo, ametaja takwimu za Klabu ambazo zimekata bima hiyo ya afya (NHIF), kuwa Kati ya Klabu 28 zilizopo, 11 tu ndiyo zimekata bima.

Pia ametaja Takwimu za waandishi wa habari ambao wamekata bima hiyo ya afya NHIF, kwa kila Press Club ambapo Kigoma wamekata 17, Mwanza 16, Mbeya 11, Shinyanga 11, Zanzibar 8, Dodoma 5.

Amesema Dar es salam waandishi waliokata bima ni 3, Rukwa 1, Simiyu 2, Katavi 2, huku akiziagiza Klabu kuendelea kuhamasisha waandishi wa habari kujiunga na vifurushi hivyo hata kwa kuchangia fedha kidogo kidogo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mgongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari.

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF Bernard Konga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari.

Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba maendeleo na makazi Anjelina Mabula akizungumza kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya NHIF kwa waandishi wa habari.

Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Deogratius Nsokolo, akizungumza kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya NHIF kwa waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Mwanza Edwin Soko, akizungumza kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya NHIF kwa waandishi wa habari.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari katika Ofisi za NHIF Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari katika Ofisi za NHIF Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari katika Ofisi za NHIF Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari katika Ofisi za NHIF Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari katika Ofisi za NHIF Jijini Mwanza.

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo, akiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya (NHIF) kwa waandishi wa habari.

Wadau wa habari wakiwa kwenye uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya (NHIF) Kwa waandishi wa habari.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akimkabidhi kadi ya bima ya afya , Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Mwanza Edwin Soko.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akimkabidhi kadi ya bima ya afya Mwandishi wa Gazeti la Nipashe mkoani Mwanza Rose Jacob, ambaye pia ni mwanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Jijini Mwanza.

Zoezi la kukabidhi Kadi za bima ya afya kwa waandishi wa habari likiendelea.

Zoezi la kukabidhi Kadi za bima ya afya kwa waandishi wa habari likiendelea.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, aliyekaa kwenye kiti katikati akipiga picha ya pamoja na wadau wa habari, Mkurugenzi mkuu wa NHIF Bernard Konga, pamoja na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kuzindua vifurushi vya bima ya afya kwa waandishi wa habari.

Na Marco Maduhu- Mwanza.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527