NEC YAMTEUA LIPUMBA KUGOMBEA URAIS TANZANIA KUPITIA CUF NA PHILIP FUMBO KUPITIA DP | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 25, 2020

NEC YAMTEUA LIPUMBA KUGOMBEA URAIS TANZANIA KUPITIA CUF NA PHILIP FUMBO KUPITIA DP

  Malunde       Tuesday, August 25, 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) na mgombea mwenza, Hamida Abdallah Huweishi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.
Profesa Lipumba ni mgombea wa saba kuteuliwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Pia, Philip John Fumbo wa chama cha DP ameteuliwa na NEC kugombea urais kwenye uchaguzi huo. Fumbo na mgombea wake mwenza, Zainabu Juma Khamisi wamekuwa wagombea wa nane kuteuliwa.

Vyama vilivyojitosa kuchukua fomu vilikuwa 17 kati ya 19 vilivyochukua fomu. Vyama ambavyo havikuchukua fomu kwenye nafasi hiyo ni TLP na UDP ambavyo vilitangaza kumuunga mkono mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli.

Shughuli ya urejeshaji fomu itahitimishwa saa 10 jioni.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post