KIGWANGALA AREJESHA FOMU YA KUOMBA KUTEULIWA KUWANIA UBUNGE WA NZEGA VIJIJINI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 14, 2020

KIGWANGALA AREJESHA FOMU YA KUOMBA KUTEULIWA KUWANIA UBUNGE WA NZEGA VIJIJINI

  Malunde       Tuesday, July 14, 2020

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala amekuwa mwanachama wa kwanza wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini.

Dkt. Kigwangalla alirejesha fomu hiyo leo ikiwa ni siku ya kwanza tangu zoezi la kuchukua fomu kwa wanachama wa CCM lilipofunguliwa.

Alisema anaomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM ili aweze kushirikiana na wachamama wa CCM katika Jimbo la Nzega Vijijini na wadau wa maendeleo katika kutatua matatizo yaliyobaki ya uboreshaji wa miundombinu.

Dkt. Kigwangalla alisema katika kipindi cha miaka mitano ndani ya jimbo hilo kumekuwepo na mafanikio makubwa ikiwemo kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria, usambazaji wa umeme wa REA kwa wananchi na ujenzi wa miundombinu ya afya.

Alisema kama akipewa fursa nyingine atajitahidi kushirikiana na Serikali na wakazi wa Jimbo hilo katika kuhakikisha wanarekebisha miundombinu ya barabara.

MWISHO


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post