CCM WAMSAMEHE NA KUFUTA ADHABU YA KATIBU MSTAAFU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 10, 2020

CCM WAMSAMEHE NA KUFUTA ADHABU YA KATIBU MSTAAFU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA

  Malunde       Friday, July 10, 2020

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemsamehe Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na kumfutia adhabu ya miezi 18 aliyokuwa akiitumikia.

Tangazo hilo limetolewa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais John Magufuli wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kinachoendelea jijini Dodoma baada ya kuomba ridhaa ya wajumbe wa kikao hicho ambao nao wameridhia Kinana asamehewe.

Rais Magufuli amesema Mzee Kinana ameonekana kujutia makosa aliyokuwa ameyatenda na kuomba msamaha, hivyo ni vema akasamehewa ili aungane na wanachama wenzake katika kukijenga chama.

Tayari Mzee Kinana ametumikia adhabu hiyo kwa muda wa miezi minne.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post