ATIWA MBARONI KWA TUHUMA YA KUSAFIRISHA SHEHENA YA DAWA ZA BINADAMU | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 14, 2020

ATIWA MBARONI KWA TUHUMA YA KUSAFIRISHA SHEHENA YA DAWA ZA BINADAMU

  Malunde       Tuesday, July 14, 2020

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Fredrick Anaclet Maxmilian (38) mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma ya kusafirisha shehena ya madawa ya binadamu sampuli 149 baadhi yakiwa na nembo ya MSD.


Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP. Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma.

Aidha Muroto amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 09/07/2020 majira ya saa moja jioni.

Amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo imeonekana kuwa yeye siyo daktari wala mfamasia na dawa ila anashirikiana na mfamasia ambaye ni mtumishi wa Serikali (jina limehifadhiwa) huko mkoani Tabora.

Kamanda Murotto amesema uchunguzi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Hoapitali ya mkoa wa Dodoma Dkt.Samuel Seseja amesema shehena hiyo ina dawa aina nane ambapo zipo zenye nembo ya Serikali,pia zipo zenye nembo ya MSD na nyingine hazina nembo.

Hata hivyo amesema dawa hizo hazitakiwi kuuzwa na mtu yeyote kwani kuna wazabuni wa kufanya kazi hiyo katika kila mkoa.

Lengo lilikuwa ni kuziuza kwenye maduka mbalimbali ya dawa jambo ambalo siyo sahihi.

“Uuzaji wa dawa unalindwa na sheria inayotoa namna gani dawa hizo ziweze kununuliwa na kuuzwa, hivyo hicho ni kinyume na sheria inayosimamia suala la dawa na vifaa tiba.”amesema Dkt.Seseja.

Alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wafanyabiashara na watoa huduma kutojihusisha na ununuzi wa dawa kutoka kwa vyanzo ambavyo havifahamiki na kwamba  wanapaswa kununua kwenye maduka ya dawa yaliyosajiliwa na mfamasia Mkuu wa Serikali.

Pia amewataka kutojihusisha na watoa huduma wasio waaminifu wanaoitia doa Serikali inayofanya kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post