TANESCO YATOA ELIMU YA MATUMIZI BORA NA SAHIHI YA UMEME KWA WACHIMBA MADINI HUMO MBEYA

  MaafisaTANESCO wakipata maelezo kutoka kwa Afisa madini wa kiwanda Cha Mdimi investment kilichoko wilayani Chunya mkoani Mbeya Joseph Mamuya wakati maafisa hao walipotembelea kiwandani hapo jana.

Na mwandishi wetu, Mbeya
SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO kupitia idara ya masoko,
limeendelea na kampeni kabambe ya kuhakikisha inatoa Elimu kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa wa madini pamoja na mashine za kusaga nafaka mkoani mbeya ili wafahamu Elimu ya matumizi Bora ya umeme.

Lengo la kampeni hiyo Ni kuhamasisha matumizi bora ya umeme,
usalama wa umeme kwa  viwanda hivyo, kuunga mkono jitihada za Mh Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha uchumi wa
viwanda unafikiwa kwa Kasi nchini na kuongeza Tija kwa Taifa.

Miongoni mwa migodi ambayo imekwishatembelewa mkoani Mbeya ni pamoja na mgodi wa makaa ya Mawe Kiwira, mgodi wa dhahabu Chunya wa Mdimi investment, Mehrab minerals resources, mgodi wa mama Today iliyoko wilayani
Chunya.
 MaafisaTANESCO wakipata maelezo kutoka kwa Afisa madini wa kiwanda Cha Mdimi investment kilichoko wilayani Chunya mkoani Mbeya Joseph Mamuya wakati maafisa hao walipotembelea kiwandani hapo jana.
 Mitambo ya kuchakata makaa ya mawe
 Maafisa wa TANESCO wakiwa kwenye moja ya viwanda walivyotembelea
Afisa mwandamizi wa ufundi kutoka TANESCO Stewartness Makiko akikagua moja ya mota zinazotumiwa na kiwanda Cha kukamua alizeti Cha Moravian kilichoko Wilaya ya chunya
 Mchimbaji mdogo wa dhahabu akisafisha mchanga kusaka madini hayo
 MaafisaTANESCO wakipata maelezo kutoka kwa Afisa madini wa kiwanda Cha Mdimi investment kilichoko wilayani Chunya mkoani Mbeya Joseph Mamuya wakati maafisa hao walipotembelea kiwandani hapo jana.
Vijana kutoka kiwanda Cha kuchakata mbao kutoka Tukuyu Cha Kapinga wakisikiliza kwa making Elimu inayohusu masuala ya umeme wakati walipowatembelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527