TANZANIA YAMTAMBULISHA MCHIMBAJI MDOGO WA MADINI YA TANZANITE KUWA BILIONEA


Wizara ya Madini leo imemtambua rasmi mchimbaji mdogo Saniniu Laizer kuwa Bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili ya Tanzanite yenye thamani ya Tsh.  Billion 7.8. 



Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila  amesema kuwa mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo” amesema Prof. Msanjila

Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.



 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post