WAZIRI MWIGULU AVITAKA VYOMBO VYA SHERIA NCHINI KUEPUKA KUTUMIKA VIBAYA

 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao cha kamati za kuratibu msaada wa kisheria na ukaguzi wa watoa huduma na msaada wa kisheria mkoani Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
 Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu akizungumza wakati wa kikao hicho
 Waziri wa Sheria na Katiba Mwigulu Nchemba katikati akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella mara baada ya kufungua kikao cha watoa huduma ya msaada wa kisheria uliofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Beach Resort mjini Tanga jana kulia ni katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na katiba Profesa Sifuni Mchome

 Sehemu ya wadau wakiwa kwenye kikao hicho
 Sehemu ya wadau wakiwa kwenye kikao hicho
Waziri wa katiba na sheria Dkt Mwigulu Nchemba katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao hicho kulia ni Katibu Wizara ya Sheria na katiba Profesa Sifuni Mchome kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Mwigulu Nchemba amevitaka vyombo vya kisheria nchini kutotumika vibaya na watu wachache kupindisha sheria kwa ajili ya maslahi yao na kusababisha uvunjifu wa haki na kuwanyima wanyonge haki zao.


Waziri Mwigulu Nchemba ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao Cha kamati za kuratibu msaada wa kisheria na ukaguzi wa watoa huduma na msaada wa kisheria mkoani Tanga.



Alisema kuwa yapo mazoea katika jamii ya watu wenye mamlaka ya kutoa au kusimamia haki kutumia vibaya mwamvuli wa kisheria ili kuweza kutimiza malengo Yao kwa kupindisha sheria.



Alisema kuwa katika Hilo kuathirika mkubwa anakuwa ni Mwananchi yule ambaye ni maskini na mnyonge na hivyo kusababisha kuvuruga maslahi mapana ya nchi katika swala Zima la haki na wajibu.



"Uwepo wa kamati hizi za msaada wa kisheria zimewekwa kwa lengo la kuwasaidia wajane ,yatima na wale wasio na uwezo kupata haki zao hivyo nendeni mkasimamie haki hizo"alisema Waziri huyo.



Aidha aliziagiza kamati za kisheria nchini kuhakikisha zinatambua changamoto za kisheria zinazowakabili wananchi kwenye maeneo yao na kuzifanyia kazi badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa kufika katika maeneo yao na kueleza kero hizo.



"Kuna wananchi ambao wanauhitaji msaada mkubwa wa kisheria lakini kutokana na kushindwa kujua wapi pa kuanzia wameshindwa kupata haki zao kwa wakati mwafaka,hivyo nendeni mkawasaidie wananchi katika Hilo"alisisitiza Waziri Nchemba.



Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome alisema kuwa uwepo wa kamati hizi ni kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wenye hali duni wanapata msaada wa kisheria ili kupata haki zao bila ya manunguniko.

"Haki lazima eindane na wajibu hivyo katika kuhakikisha nchi inakuwa na amani ni wajibu wa serikali kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi wao kupata haki bila ya kudhulumiwa"alisema Prof Mchome.


Hata hivyo Msajili wa msaada wa kisheria mkoa wa Tanga Emil Mashauri alisema kuwa uwepo wa kamati hiyo inalengo la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanyonge ambao wanakosa huduma hiyo.

Alisema kuwa migogoro mingi inatokea katika jamii kutokana na jamii kutokujua sheria hivyo kamati kwa kushirikiana na paralegal wataweza kusaidia wananchi hasa wanyonge kukabiliana na changamoto ya kupata haki zao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela alisema kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ni kero ya mirathi pamoja na migogoro ya ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa inahitaji tafsiri za kisheria hususani kwa wananchi wa Hali ya chini.

Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo tayari amewaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huu kila wapo fanya mikutano Yao kujadili maendeleo wawe na kipengele Cha msaada wa kisheria ili kuweza kutatua kero za kisheria zinazowakabili wananchi.

"Niwaombe wajumbe wa kamati kuweka utaratibu wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na msaada wa kisheria katika nyanja mbalimbali "alisema RC Shigela.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527