YANGA YAMPIGA FAINI YA MILIONI 1.5 MCHEZAJI WAKE BENARD MORRISON


Uongozi wa klabu ya Yanga umempiga faini ya Sh. 1.5 Milioni nyota wake raia wa Ghana, Benard Morrison kwa kufanya mahojiano na mwandishi wa habari bila kutoa taarifa kwa klabu na kuzua hali ya sintofahamu juu ya mkataba wake. 


Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga imeeleza kuwa mchezaji huyo aliingia mkataba wa kwanza na timu hiyo tarehe 15 Januari, 2020,  kwa muda wa miezi sita huku kukiwa na kipengele cha kuongeza kama wataridhishwa na kiwango chako.

Klabu imeendelea kwa kueleza kuwa walimuongezea mchezaji huyo mkataba wa mara pili terehe 20 Machi, 2020 ukiwa mkataba wa miaka miwili ambao utafikia kikomo tarehe 14 Julai, 2022. Mbele ya mwana sheria wa klabu ya Yanga pamoja na mwakilishi kutoka GSM, mhandisi Hersi Said.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527