MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA YAKUBALI MBUNGE SULEIMAN NCHAMBI NA MKEWE WAPEWE DHAMANA


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 15,2020 imekubali ombi la Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoa wa Shinyanga Suleiman Nchambi (CCM) na mkewe Aisha Khalfan Masoud wapewe dhamana.Akitoa maamuzi ya maombi ya dhamana hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Phocus Mkeha, ambaye alikuwa akisikiliza maombi ya dhamana hiyo amesema Mbunge huyo ana haki ya kupewa dhamana kwa masharti ya kusaini bondi ya Shilingi Milioni 50, na mdhamini wake bondi ya Shilingi Milioni 10, pamoja na kushikiliwa Hati yake ya kusafiria 'Passport'.


Aidha amesema maamuzi ya utoaji wa dhamana hiyo ameyarudisha katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga mahali kesi yake ya msingi ilipoanzia ambapo wao ndiyo watasimamia masharti ya utoaji wa dhamana hiyo.

Mbunge Suleiman Nchambi ashtakiwa kwa makosa 12 ya Uhujumu Uchumi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527