VIONGOZI WA TFF WAHOJIWA NA TAKUKURU KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZIKIWEMO ZILIZOTOLEWA NA RAIS MAGUFULI


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imewataka maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kuzirejesha fedha walizochukua kabla hatua nyingine hazijafuata.

Hatua hiyo imekuja baada ya TAKUKURU kudai Shirikisho  limekuwa na matumizi mabaya ya fedha ikiwemo fedha zilizotolewa na Rais  Magufuli kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON ya Vijana chini ya Miaka 17 yaliyofanyika mwaka jana hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Brig. John Mbungo amesema taasisi hiyo imeamuru maofisa hao wa TFF kurudisha fedha hizo kabla hatua nyingine hazijafata baada ya kupata ushahidi wa nyaraka mbalimbali.

Mbungo amesema, wanajiandaa kuwahoji baadhi ya maofisa wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF   kwa matumizi mabaya ya fedha ikiwemo fedha zilizotolewa na Raisi Magufuli billioni moja kwaajili ya maandalizi ya mashindano ya vijana Afrika,U17 yaliyofanyika mwaka jana hapa nchini.

Amesema,kuna baadhi ya maofisa wengine wa TFF wamehojiwa na baadhi ya nyaraka zimechukuliwa na wale waliobainika kuchukua fedha hizo wana hiari ya kuzirejesha kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527