MBUNGE AIOMBA SERIKALI KUMSHUGHULIKIA WAZIRI WA ZANZIBAR ALIYEDAIWA KUGOMA KUKAA KARANTINI YA CORONA

Mbunge wa Konde(CUF) Khatib Said Haji ameiomba Serikali kumchukulia hatua Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa kwenye karantini na kusababisha maambukizi kwa watu wawili kwenye familia yake.


Akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 amesema matokeo ya Hilo nyumbani kwake kuna watu wawili amewaambukiza na huko hospitali haijulikani matokeo yake nini.

“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa sana. Baada ya malalamiko makubwa ndio alikubali kuwekwa kwenye karantini,”amesema.

Amesema alifanya hivyo kwa sababu ya kiburi cha madaraka yake na kumpongeza makamu wa pili wa Rais Zanzibar kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.

“Huu ndio utu, huu ndio ubinadamu leo waziri huyu ni nani anayekataa uamuzi wa Serikali hata uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Hatuwezi kumchekea mtu mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu ni waziri ulichukulie hatua haraka."


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527