MAJESHI YA UTURUKI YADUNGUA NDEGE MBILI ZA KIVITA ZA SYRIA


Vikosi vya Uturuki vimedungua ndege mbili za kivita za serikali ya Syria katika mkoa wa kaskazini-maghribi wa Idlib siku ya Jumapili, baada ya Ankara kutangaza operesheni ya kijeshi ndani ya mipaka ya Syria.


Shirika la uangalizi wa haki za binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza, lilisema ndege hizo mbili chapa ya Sukhoi zilianguka katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya utawala, baada ya kushambuliwa na ndege za Uturuki aina ya F-16.

Shirika la habari la serikali ya Syria SANA, lilisema vikosi vya Uturuki "vimelenga" mbili kati ya ndege zake kaskazini-magharibi mwa Syria. T

angu Desemba, vikosi vya utawala vikiungwa mkono na Urusi vimeongoza operesheni ya kijeshi dhidi ya ngome ya mwisho ya waasi ya Idlib, ambako Uturuki inayaunga mkono baadhi ya makundi ya waasi.

Wizara ya ulinzi ya Uturuki pia iliripoti kudunguliwa kwa ndege hizo siku ya Jumapili, lakini haikuthibitisha juu ya nani alihusika. "Ndege mbili za utawala za SU-24 zilizokuwa zinashambulia ndege zetu zimeangushwa," ilisema.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Uturuki kutangaza operesheni ya kijeshi kaskazini-magharibi mwa Syria baada ya mashambulizi ya ndege za utawala wa Syria kuuwa wanajeshi  zaidi ya 30 wa Uturuki siku ya Alhamisi.

Mashambulizi ya kisasi ya ndege zisizo na rubani na mizinga yameuwa wanajeshi 74 wa Syria na wapingaji 14 washirika tangu siku ya Ijumaa, limesema shirika la uangalizi wa haki za binadamu. Pia Jumapili jeshi la Syria lilianguisha ndege ya Uturuki isiyo na rubani kaskazini-magharibi mwa Syria.

Shirika la SANA lilisema ndege isiyo n rubani ilidunguliwa karibu na mji wa Saraqeb, na kuchapicha picha za ndege ikiporomoka kutoka angani ikiwaka moto. 

Shirika la haki za binadamu pia lilithibitisha tukio hilo. Jeshi la Syria lilikuwa limeonya kwamba lingedungua ndege yoyote inayokiuka anga yake kaskazini-magharibi mwa Syria.

-DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527