CCM WAELEKEA MAHAKAMANI KUMLIPIA FAINI DKT VICENT MASHINJI...ALIHUKUMIWA JANA PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA


Katibu wa itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufuata utaratibu, wa kulipa faini ya Sh milioni 30 ili kumnusuru DK Vicent Mashinji aliyetiwa hatiani jana.


Akizungumza katika viwanja vya mahakama akiwa ameambatana na wanachama wengine wa chama hicho pamoja na mke wa mfungwa huyo , Polepole amesema amefika kufuata utaratibu ili wamtoe Mashinji.

"Tunaishukuru CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wametusaidia tangu jana mpaka saa 4:00 usiku, tulikuwa tumekusanya kiasi chote kilichokuwa kinahitajika mahakamani ili kumnusuru ndugu yetu Mashinji, sisi hatuna mashaka na yeye na wala hatutomshikia bango kwamba tulimchangia na hata akiondoka wiki ijayo hatutohuzunika.


“Tayari tumeshapewa control namba, tunaenda kulipa kisha tutarudi Mahakama ya Kisutu ili tupewe utaratibu wa kwenda kumtoa gerezani,” amesema Polepole.

Dkt Vicent Mashinji pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA, katika kesi yao ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana walihukumiwa kulipa faini ama kwenda jela miezi mitano, ambapo faini ya Mashinji ni Milioni 30.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post