WAZIRI WA AFYA UINGEREZA AAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA


Waziri wa afya na mbunge wa chama cha Conservative nchini Uingereza Nadine Dorries ametangaza kuwa ameambukizwa virusi vya corona. 


Dorries, ambaye ni mbunge wa kwanza kugunduliwa na homa hiyo hatari, alisema alichukua tahadhari zote baada ya kubaini kuwa ameathirika, na amejiweka karantini nyumbani kwake.

Hali hii imekuja wakati kukiwa na taarifa ya kifo cha mtu wa sita kutokana na virusi vya corona nchini Uingereza .


Bi Dorries, mbunge wa Bedfordshire ya kati, amesema katika taarifa yake kuwa Idara ya afya imeanza kuwafuatilia watu waliokuwa karibu naye, na ofisi yake ya bunge inafuatilia hilo kwa karibu.

Alieleza kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu hali aliyokuwa nayo, lakini akielezea hofu aliyonayo kuhusu mama yake ,84, anayeishi naye ambaye naye ameanza kukohoa siku ya Jumanne.



-BBC


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527