WALIMU WATATU WAUAWA KWA SHAMBULIZI LA KIGAIDI KENYA



Watu watatu wameuawa baada ya wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab kuvamia mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa huku kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.
Maafisa wa polisi wanafuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama zikionyesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo.

Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.

Wiki iliyopita, Uingereza imetoa onyo kwa raia wake wanaotaka kusafiri nchini humo dhidi ya kutembelea kaunti ya Garissa na katika eneo la ndani ya kilomita 60 katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Hili ni shambulizi la 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi 4 yakitekelezwa Garissa, 3 Wajir, 2 Mandera na 2 Lamu.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527