MASHAMBULIZI YA ROKETI YAFANYWA KWENYE MAKAZI YA WANAJESHI WA MAREKANI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, January 13, 2020

MASHAMBULIZI YA ROKETI YAFANYWA KWENYE MAKAZI YA WANAJESHI WA MAREKANI

  Malunde       Monday, January 13, 2020

Jeshi la Iraq limesema karibu makombora sita yamerushwa katika kambi ya kijeshi ya Balad kaskazini mwa Mji Mkuu wa Baghdad leo na kuwajeruhi wanajeshi wanne wa Iraq. 


Kambi hiyo ambayo iko kilomita 80 kaskazini mwa mji huo mkuu ni makao ya majeshi ya Marekani pia ingawa kiasi kikubwa cha wanajeshi wa Marekani walikuwa washaondolewa na kupelekwa kwengine kutokana na mvutano unaozidi kati ya Marekani na Iran.

 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema ameghadhabishwa na ripoti za mashambulizi hayo. 

Taarifa kutoka kwa jeshi la Iraq imesema roketi nane zimerushwa katika kambi hiyo ya kijeshi jana na kuangukia katika njia ya ndege na lango la kambi hiyo. 

Hakuna aliyekiri kuhusika na mashambulizi hayo kufikia sasa. Hakuna aliyeuwawa katika mashambulizi hayo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post