RAIS UHURU KENYATTA ASEMA WAKILI MIGUNA YUKO HURU KUREJEA KENYA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 31, 2019

RAIS UHURU KENYATTA ASEMA WAKILI MIGUNA YUKO HURU KUREJEA KENYA

  Malunde       Tuesday, December 31, 2019

Rais Uhuru Kenyatta amesema wakili aliyetimuliwa  nchini Kenya  Miguna Miguna yuko huru kurejea Kenya kwani ni haki yake Kikatiba.

Kiongozi  huyo wa taifa alisema Miguna ataruhusiwa kurejea nchini lakini atumie uhuru wake wa kujieleza kueneza amani na umoja miongoni mwa Wakenya.

Akizungumza katika hafla ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe Charles Rubia katika Kaunti ya Murang’a mnamo Jumatatu, Desemba 30, Uhuru alisema serikali yake itatoa uhuru kwa Wakenya wote kama ilivyopiganiwa na viongozi waliotangulia.

“Hakuna mtu ambaye amezuiwa kusema yale anayotaka kusema. Ata nasikia kuna wengine wanataka kupanda ndege warudi..waendelee..hio ni uhuru wao," alisema kiongozi huyo wa chama cha Jubilee.

Wakili Miguna anatazamiwa kuingia nchini Jumanne 7, Januari 2020.

Wakili huyo alitangaza kuwa atarejea nyumbani kupitia ukurasa zake za utandawazi siku ya Alhamisi, Desemba 19.

“Narejea nyumbani. Haki ya kuzaliwa, Haki ya Katiba na amri ya korti. Mabadiliko kwa ushawishi. Nitawasili: Jumanne, Januari 7, 2020 mwendo wa saa tatu na dakika 25 usiku kupitia ndege ya Lufthansa LH 590,” aliandika Miguna kwenye Twitter.

Wakili huyo alitimuliwa Kenya  kwa mara ya kwanza Februari 2018 baada ya kumuapisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kama rais wa watu mnamo Jumanne, Januari 30 katika bustani ya Uhuru.

Mnamo Machi 2018, juhudi zake za kuingia nchini ziliambulia patupu huku serikali ikisema kwamba aliasi uraia wake wa Kenya ili kuwa raia wa Canada.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post