TUME YA UCHAGUZI YATOA MWALIKO KWA TAASISI NA ASASI ZA KIRAIA KUTOA ELIMU KWENYE UCHAGUZI MKUU WA 2020


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imetoa nafasi kwa taasisi au asasi zenye nia ya kutoa elimu ya mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 kuwasilisha maombi yao kwa tume hiyo.


Taarifa iliyotolewa Novemba 22, 2019 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Gerald Mwanilwa imesema hatua hiyo inatokana na kifungu cha 4C cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura ya 343 kinaeleza Tume ina jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa elimu hiyo.

Mwanilwa amebainisha vigezo ni; taasisi au asasi itakayowasilisha maombi hayo inatakiwa kuwa na usajili kwa mujibu wa sheria za taifa, iwe imefanya kazi nchini si chini ya miezi sita tangu kusajiliwa kwake.

Vingine ni; asasi au taasisi iwe haina taarifa ya kuvuruga amani au kuchochea fujo ndani ya nchi na nchi nyingine, iwe tayari kujigharamia katika kutoa elimu ya mpiga kura na watendaji wake wakuu watatu, wawili wanapaswa kuwa Watanzania.

Kaimu mkurugenzi huyo amesema maombi hayo yanatakiwa kuambatanishwa na cheti cha usaili, katiba ya taasisi au asasi, majina ya viongozi wakuu wa taasisi au asasi, anuani kamili ya makazi na ratiba kamili ya maeneo wanayotarajia kutoa elimu kwa mpiga kura.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527