MAJAJI WATATU KUTUMIA WIKI 3 KUSIKILIZA MASHAURI 29


Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kuwasilishwa na kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa ambayo inaanza leo Jumatatu Novemba 25 hadi Desemba 11, 2019 Kisiwani Unguja, Zanzibar.   


Mashauri ya rufaa za madai ni 12, mashauri ya jinai matatu, mashauri ya madai 11 na maombi ya jinai ni matatu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa Amir Khamis Msumi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Msumi amesema kikao hicho cha wiki tatu kitaongozwa na majaji watatu ambapo Mwenyekiti wao atakuwa Jaji Agostona Mahija akisaidiana na Jaji Gerad  Ndika pamoja na Jaji Rehema Kerefu.

Amesema kikao hicho  kimepanga kusikiliza mashauri yote na ikiwezekana kuyatolea uamuzi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post