MIKOA YA KANDA YA ZIWA YATIKISA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019

Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambako mikoa ya kanda ya ziwa imeonekana kuongoza.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya shule 10 bora kitaifa zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo mikoa ya  Mara,Shinyanga,Kagera,Mwanza.

Kwa upande wa Watahiniwa bora kitaifa nafasi ya Kwanza imechukuliwa na mtahiniwa kutoka mkoa wa  Mara,nafasi ya pili Geita, nafasi ya tatu mkoa wa Dar es salaam (siyo Kanda ya Ziwa),nafasi ya nne,tano,sita ni Mara, saba Shinyanga, nane Mwanza,tisa Shinyanga na kumi Mara.
ANGALIA HAPA MATOKEO DARASA LA SABA 2019


Soma pia hizi↡↡↡↡
Breaking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA MWAKA 2019

KAULI YA UONGOZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA, YA KWANZA KIMKOA MATOKEO DARASA LA SABA 2019



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527