KAULI YA UONGOZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA, YA KWANZA KIMKOA MATOKEO DARASA LA SABA 2019


Muonekano wa madarasa ya shule ya msingi Little Treasures
Jengo la utawala shule ya msingi Little Treasures

Hii hapa kauli ya Uongozi wa Shule ya Little Treasures baada ya kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019.


"Kwa niaba ya Familia ya Little Treasures napenda kutumia fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake kwetu sote! Pia tunawashukuru viongozi wa dini  mbalimbali kwa sala na maombi yao.

Pili, kwa namna ya kipekee niwashukuru viongozi wetu wote wa serikali kwa kuwa bega kwa bega na shule yetu,wamekuwa washauri wazuri  katika kuifanya  Little Treasures kuwa shule bora.  Pia tunapenda kuwashukuru sana wazazi na walezi wa wanafunzi wetu kwa ushirikiano wao na shule katika kufikia malengo yetu. 

Hali kadhalika shukrani ziwaendee watumishi wote wa LTS ambao wametumia muda wao mwingi katika kuwalea na kuwapa maarifa mbalimbali wanafunzi wetu. 

Na pia kwa nafasi hii tunapenda kuwapongeza wanafunzi wetu kwa utayari wao katika kujifunza na umakini wao katika mitihani na hatimaye kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba 2019 ngazi ya wilaya,kimkoa na kitaifa.

Mwisho, Tunawashukuru sana wadau wote ambao mmekuwa mkishirikiana nasi kuifanya Little Treasures kuwa mahali pazuri kwa watoto wetu. Naomba tuendelee kushirikiana kwa matokeo mazuri zaidi. Mungu ibariki LTS ! Mungu Ibariki Tanzania!  Mungu tubariki sote.

Mkurugenzi Little Treasures - Lucy Dominic👏👏👏"


Shule ya Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imekuwa shule ya nne kati ya shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 .

Nafasi ya kwanza kitaifa imeshikwa na shule ya Graiyaki,nafasi ya pili shule ya Twibhoki na nafasi ya tatu Kemebos,nafasi ya tano Musabe,sita Tulele,saba Kwema Modern ya Shinyanga,nane Peaceland, tisa Mugini na kumi Rocken Hill ya Shinyanga.

Katika matokeo hayo, Mwanafunzi Daniel Ngassa Daniel kutoka shule ya Little Treasures ameshika nafasi ya saba kitaifa.
Mbali na kushika nafasi ya nne ngazi ya taifa,Shule ya Little Treasures pia imekuwa shule ya kwanza katika ngazi ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,nafasi ya kwanza ngazi ya mkoa


Soma pia hizi↡↡↡↡
Breaking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA MWAKA 2019


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527