DC MBONEKO : WANAFUNZI LITTLE TREASURES WALINIAHIDI KUFANYA VIZURI ,KUSHANGAZA MATOKEO DARASA LA SABA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko ameipongeza shule ya Msingi Little Treasures kwa kuwa shule ya nne kitaifa kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba 2019 yaliyotangazwa leo Jumanne Oktoba 15,2019.

Shule ya Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imekuwa shule ya nne kati ya shule 10 bora kitaifa ambapo nafasi ya kwanza imeshikwa na shule ya Graiyaki,nafasi ya pili shule ya Twibhoki na nafasi ya tatu Kemebos,nafasi ya tano Musabe,sita Tulele,saba Kwema Modern ya Shinyanga,nane Peaceland, tisa Mugini na kumi Rocken Hill ya Shinyanga.

Katika matokeo hayo, Mwanafunzi Daniel Ngassa Daniel kutoka shule ya Little Treasures ameshika nafasi ya saba kitaifa.

Akizungumzia kuhusu matokeo hayo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amesema sababu kuu iliyofanya shule ya Msingi Little Treasures kufanya vizuri kwenye Mtihani wa Darasa la saba 2019 ni kutokana na ufundishaji mzuri wa walimu na watoto wenyewe walikuwa tayari kufanya vizuri kwenye mtihani.

"Uzuri watoto wenyewe waliniahidi kwamba watafanya vizuri kwenye mtihani,niliwauliza mwenyewe bila kupepesa macho wakasema 'Tutafanya vizuri na tutawashangaza'.Kwa hiyo wanafunzi Wame Keep the Promise",

"Tunawapongeza sana Little Treasure wametunyanyua kama wilaya ya Shinyanga na pia wameutangaza vizuri mkoa wetu wa Shinyanga.Tunawasihi na wengine waongeze bidii kwa sababu hawa watoto wenyewe walikuwa tayari",amesema Mboneko.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa shule ya Little Treasures Lucy Dominic ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo akisema walitarajia matokeo mazuri kwa wanafunzi wao kutokana na kuwaandaa vizuri.

"Nimepokea kwa furaha matokeo ya Mtihani Darasa la saba 2019.Tumeshika nafasi ya 4 kitaifa.Siri kubwa ni kwamba watoto waliandaliwa vizuri na yalikuwa ni matarajio yetu kwa uwezo wa Mungu kuwa wanafunzi wetu watafanya vizuri",amesema Dominic.

ANGALIA HAPA MATOKEO DARASA LA SABA 2019



Soma pia hizi↡↡↡↡
Breaking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA MWAKA 2019

KAULI YA UONGOZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA, YA KWANZA KIMKOA MATOKEO DARASA LA SABA 2019



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527