AJALI YA LORI YAUA WATU WAWILI KATAVI



Na Walter Mguluchuma - Malunde 1 blog
Watu wawili wamekufa hapo hapo na wawili kujeruhiwa  baada ya gari aina ya Scania waliokuwa wakisafiria kupinduka  katika kijjii cha Mirumba kata ya Kibaoni tarafa ya Mpimbwe wilaya ya Mlele  mkoa wa Katavi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga amesema ajari hiyo imetokea leo majira ya saa tisa mchana katika kijiji cha Mrumba barabara ya kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda Mkoani Katavi.

Kamanda Kuzaga aliwataja watu wawili waliokufa baada ya gari hilo kupinduka kuwa ni Seleman Said Seleman( 50) mkazi wa Dares salaam na ambaye ni   dereva wa gari hilo na Chalo Charles(26) mfanyabiashara wa mazao mkazi wa kijiji cha Igurubi Tabora.

Majeruhi amewataja kuwa ni Abdallah Said Kongo tingo wa gari hilo mkazi wa Kigamboni Dare s salaam ambaye ameumia ameumia katika sehemu mbalimbali za mwili wake na Edward Mazoya (30) mkazi wa Mwanza ambaye naye ameumia sehemu mbalimbali za mwili.

Kamanda Kuzaga alisema ajali hiyo ililihusisha gari lenye namba za usajili AZB 596 aina ya Scania mali ya Godbless Shoo wa Mwanza lililokuwa likiendeshwa na Seleman Said Seleman ambaye amepoteza maisha.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva na  kushindwa kuchukua tahadhari kwenye mlima baada ya kuwa ametumia pombe kali wakati akiendesha gari hilo.

Alisema kabla ya kupata ajari hiyo dreva wa gari hilo alikuwa amekunywa pombe nyingi kupita kiasi katika eneo la kijiji cha Kizi wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambapo eneo hilo la Kiza ni maarufu kwa kuuza vinywaji vikali na chakula.

Majeruhi wote wawili wamelazwa katika kituo cha afya Usevya na  hali zao zikiwa sio nzuri na miili ya marehemu imehifadhiwa kituo cha afya Usevya.

Kamanda kuzaga ametoa wito kwa kwa madereva na wamiliki wa magari kufuata taratibu za sheria za usalama wa barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527