Picha : SHIRIKA LA 'KWA WAZEE NSHAMBA' LATOA MSAADA WA BAISKELI 100 KWA WANAFUNZI WA KIKE VITA DHIDI YA MIMBA ZA UTOTONI

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Shirika lisilo la kiserikali la Kwa Wazee Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera limetoa msaada wa baiskeli  100 zenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa  wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za sekondari 25 wilayani  humo ili kuwawezaesha wanafunzi hao  kupata elimu bila vikwazo.

Zoezi hilo la ugawaji wa baiskeli bure kwa wanafunzi hao kutoka  shule 25 za sekondari za wilaya ya Muleba hiyo limefanyika leo Septemba 20, 2019 katika  uwanja wa Zimbihile wilayani humo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi hasa wale wanaotembea umbali mrefu kwenda shule na kupunguza mimba za utotoni zinazotokana na vishawishi wavipatavyo njiani.

Meneja wa mradi wa  Vijana Bicycle Center (VBC) chini ya shirika la kwa wazee Nshamba Adelphinus Alexander amesema  wilaya ya Muleba imekuwa ikitajwa mara kwa mara kuhusika na vitendo vya mimba za utotoni jambo ambalo husababisha watoto wa kike kushindwa kufikia ndoto zao huku wengi  wakiishia katika vishawishi vya kupewa lifti na waendesha pikipiki ambao huharibu maisha yao kabla ya kutimiza ndoto zao.

Ameeleza kuwa kufuatia hali hiyo shirika hilo limeamua kupambana vikali ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo kwa kutoa baiskeli 100 kwa watoto hao wa kike kutoka shule za sekondari 25 za wilaya hiyo ambapo pia zimetolewa taa za solar 240,  mashine 26 za kuongeza usikivu kwa watooto wenye ulemavu pamoja bima za afya zipatazo 60 kwa wanafunzi  kwa ajili ya kujisomea  vitu vinavyokamilisha jumla ya shilingi milioni 23.

Mkurugenzi  wa shirika la Kwa Wazee Nshamba Lydia Lugazia amesema shirika hilo limekuwa ni mdau wa maendeleo wilayani hapo kwa kipindi cha miaka 16 ambapo licha ya kujizatiti katika huduma za kuongeza kinga kwa jamii, ikiwemo  kutetea , kulinda na kusaidia wazee na watoto  lengo lao ni kuongeza ustawi  kisaikolojia katika kuhakikisha watoto wote wananufaika  katika sekta ya elimu.

Lugazia amesema shirika hilo limekuwa likitoa vifaa vya shule kwa watoto wenye mahitaji maalum ambapo jumla ya walengwa 107 wakiwa wasichana 56 wavulana 51 wanahudumiwa ndani ya kata ya 6 ambazo ni Ngenge, Biirabo, Mubunda, Kashasha, Nyakatanga na Mshabago.

Kwa upande wake,Mgeni rasmi katika zoezi hilo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha amelishukuru shirika hilo katika mapamabano hayo yanayolenga kutokomeza mimba za utotoni na kuyataka mashirika mengine kuiga mfano kama huo na huku akiwahimiza  wazazi wa wanafunzi hao kutotumia baiskeli hizo katika shughuli zao binafsi bali zitumike kwa wanfunzi hao  tu kwenda shule ili kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo wadau wa elimu na wazazi wa wanafunzi hao wamewahimiza watoto hao kusoma kwa bidii na kuwa na neno hapana Mdomoni mwao mara wanapokutana na vishawishi vya aina mbalimbali.


Mgeni rasmi katika zoezi hilo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Kwa Wazee Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera kwa  wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za sekondari 25 wilayani  humo ili kuwawezaesha wanafunzi hao  kupata elimu bila vikwazo. Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mkurugenzi  wa shirika la Kwa Wazee Nshamba Lydia Lugazia akielezea namna shirika hilo limekuwa mdau wa maendeleo wilayani Muleba kwa kipindi cha miaka 16 sasa.
Meneja wa mradi wa  Vijana Bicycle Center (VBC) chini ya shirika la Kwa Wazee Nshamba Adelphinus Alexander akielezea kuhusu utekelezaji wa mradi huo wilayani Muleba.
Sehemu ya baiskeli 100 zilizotolewa na shirika  Kwa Wazee Nshamba.
Sehemu ya baiskeli 100 zilizotolewa na shirika  Kwa Wazee Nshamba.
Mashine 26 kwa ajili ya kuongeza usikivu kwa watoto wenye ulemavu zilizotolewa na Sehemu ya baiskeli 100 zilizotolewa na shirika  Kwa Wazee Nshamba.

Taa za solar 240 kwa ajili wa wanafunzi kujisomea zilizotolewa na na shirika  Kwa Wazee Nshamba.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule 25 za sekondari wilayani Muleba wakiwa eneo la tukio
Mkurugenzi  wa shirika la Kwa Wazee Nshamba Lydia Lugazia akimuonesha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha taa za solar kwa ajili ya wanafunzi kujisomea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha akijandaa kukabidhi taa za solar kwa ajili ya wanafunzi kujisomea.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha akikabidhi taa za solar kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha akifungua zoezi la ugawaji wa baiskeli 100 zilizotolewa na shirika la kiserikali la Kwa Wazee Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera zenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za sekondari 25 wilayani Muleba.  
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha akiendesha baiskeli.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba  Chrizant Kamugisha akikabidhi baiskeli kwa mmoja wa wanafunzi hao.

Wanafunzi wakiwa na baiskeli walizokabidhiwa.
Mwanafunzi akitoa neno la shukrani baada ya kupokea baiskeli.

Mwanafunzi akitoa neno la shukrani baada ya kupokea baiskeli.



Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527