ALLIANCE FC WAENDELEA KUNG'ANG'ANIWA NYUMBANI, WATOKA SARE NA BIASHARA UNITED





Na Fabian Fanuel - Malunde1 blog Mwanza
Timu soka ya Alliance FC kutoka Mwanza leo imetoka sare kwa kufungana goli 1-1 na timu ya Biashara United katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Alliance FC walikuwa wa kwanza kuliona goli la Biashara mnamo dakika ya 10 kipindi Cha kwanza huku Biashara United wakipata goli la kusawazisha dakika 43 kipindi Cha kwanza.

Baada ya mchezo kumalika Kocha Msaidizi wa Alliance FC Habibu Kondo alisema timu haijacheza vizuri ila watajitahidi kurekebisha makosa ila mechi ijayo ipate matokeo.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa timu ya Biashara Amri Said alisema kuwa wachezaji wake wameshindwa kucheza vizuri kutokana na uchovu waliokuwa nao.

Hii ni mechi ya tatu kwa timu ya Alliance FC baada ya kuanza kucheza na Mbao FC ya Mwanza na kutoa sare 1-2 na mechi ya Pili wakicheza na Kagera Sugar huku katika mchezo huo wakipoteza kwa kufunga goli 2-1 Uwanja wa Nyamagana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527