MUME ACHINJA MKE KISHA NAYE KUJIUA ..... 'WALITISHIANA KUUANA'

 Mwanaume mmoja amemchinja mke wake na kisha yeye mwenyewe kujinyonga, wakiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Nakunga, nchini Kenya.



Polisi nchini Kenya walisema tukio hilo lilitokea jana Jumapili asubuhi Agosti 18,2019.

Jirani wa wanafamilia hao, Kennedy Barasa alisema saa 3 asubuhi alisikia mayowe kutoka kwa Stephen Kagumo na mkewe Caren Chebet yaliyodumu kwa dakika kadhaa hivyo kuamua kwenda eneo la tukio kwa lengo la kutoa msaada.

Hata hivyo, Barasa alisema walipofika katika nyumba hiyo walikuta mlango umefungwa kwa ndani.

“Tulivunja mlango na kumkuta mwanamke yuko katika dimbwi la damu na mwili wa mumewe ulikuwa ukining'inia katika chumba kingine,”alisema.

Dada wa mwanaume huyo ambaye anaishi nyumba moja na wanandoa hao pamoja na mtoto wa miaka 18, alisema alipoamka alisikia shemeji yake akilumbana na mkewe.

"Nilijaribu kusogea na kumuona shemeji akiwa ameshika panga huku akigombana na mke wake. Nilisikia wakitishiana kuuana lakini baada ya muda mfupi sikusikia kitu,” alisisitiza.

Alisema baada ya majirani kufika katika chumba hicho walivunja mlango na kukuta wote wamefariki dunia.

Miili hiyo ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kitale.
Via > Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527