BINTI ALIYEMALIZA SHULE AKIWA NA UJAUZITO AUA MTOTO WAKE KISHA KUJINYONGA


Na Rehema Matowo - Mwananchi 
 Efrazia Maneno (22), mkazi wa kijiji cha Nyaseke kata ya Bulela mjini Geita nchini Tanzania anadaiwa kumuua kwa kumnyonga mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili kwa kitambaa kisha naye kujinyonga.

Tukio hilo limetokea jana Jumapili Agosti 18, 2019 saa saba mchana umbali wa mita 300 kutoka nyumba aliyokuwa akiishi, alitumia khanga kujinyonga katika mti wa mwembe.

Maneno Kapunda, baba mzazi wa Efrazia amedai binti yake alikuwa akiishi na babu na bibi baada ya wazazi kutengana na hakueleza tatizo lolote kabla ya kufanya uamuzi wa kujiua

“Huyu binti yangu alimaliza shule ya Sekondari Bulela akiwa mjamzito na mwanaume aliyempa mimba alikataa hivyo alibaki hapa nyumbani na wazee kwa kweli tukio hili limenishangaza,” amesema Kapunda

Ofisa mtendaji wa kijiji cha Nyaseke, John Maguta amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi walifika jana jioni Jumapili na kutoa mwili uliokuwa ukining’inia na kuruhusu familia kuendelea na taratibu za mazishi.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post