Picha : WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS' WAPIGWA MSASA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 17, 2019

Picha : WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS' WAPIGWA MSASA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

  Malunde       Wednesday, July 17, 2019
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism' ili waweze kuandika kwa weledi habari zinazohusu utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.

Mafunzo hayo ya Waandishi hao wa habari mitandaoni yanafanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku mbili Julai 17,2019 hadi Julai 18,2019 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi huo unatekelezwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania  kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism'. Picha zote na Kadama Malunde na Albert G. Sengo
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akitoa mada wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akisikiliza hoja kutoka kwa Mshiriki wa mafunzo hayo,William Bundala wa Kijukuu blog wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV).
Mwezeshaji katika mafunzo ya Uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akiendelea na mada ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakioneshana kitu kwenye Laptop
Mafunzo yanaendelea.
Endelea kuangalia picha za matukio mbalimbali ukumbini
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi 'Investigative Journalism'. Picha zote na Kadama Malunde na Albert G. Sengo.

Soma pia :WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS/ONLINE TV' WAPEWA MAFUNZO YA HAKI ZA KATIBA NA SHERIA ZA HABARI
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post