Picha : WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI 'BLOGGERS/ONLINE TV' WAPEWA MAFUNZO YA HAKI ZA KATIBA NA SHERIA ZA HABARI


Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania wamepatiwa mafunzo kuhusu haki za Katiba na sheria  za habari ikiwemo Sheria ya Takwimu 2015, Sheria za Huduma za Habari 2016 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 ili kuwajengea uwezo wa kuandika  kwa weledi habari za utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.


Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Mei 21,2019 yamefanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli jijini Dodoma, yameandaliwa na 
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT ambapo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mei 21,2019: Wakili James Marenga akitoa mada kuhusu sheria ya Maudhui Mtandaoni 'The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations ,2018' wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mtandaoni 'Bloggers/Online Tv' 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Wakili James Marenga akiendelea kutoa mada ukumbini.
Wakili James Marenga akitoa mada ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.

Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Mei 22,2019: Wakili James Marenga akitoa mada kuhusu sheria ya huduma za habari 'The Media Services Act No. 12,2016' wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari mtandaoni 'Bloggers/Online Tv' 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Wshiriki wa mafunzo hayo wakiandika dondoo muhimu wakati Wakili James Marenga akitoa mada ukumbini.

Kushoto ni Albert G. Sengo (GSengo Blog) na Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko wakiwa ukumbini.

Picha ya pamoja Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Picha ya pamoja waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

Soma pia >WAANDISHI MTANDAONI 'BLOGGERS' WAKUTANA DODOMA KUJADILI MPANGO KAZI WA MRADI WA UTETEZI NA USHAWISHI WA HAKI ZA BINADAMU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post