MAKAMBA AWATOA HOFU WAUZA KARANGA, UBUYU, ICE CREAM | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 15, 2019

MAKAMBA AWATOA HOFU WAUZA KARANGA, UBUYU, ICE CREAM

  Malunde       Saturday, June 15, 2019
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba imesema hakuna mtu atakayekamatwa kwa kukutwa na vifungashio vya vyakula mfano wa karanga, Ubuyu, kwani kinachokatazwa ni kutumia vifungashio hivyo kubebea bidhaa nyingine.

Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya kusambaa habari kuwa Serikali imepiga marufuku matumizi ya vifungashio vinavyohifadhia vyakula kama ubuyu, karanga, ice cream.

“Vifungashio vya bidhaa za vyakula (karanga, ubuyu, etc) havijazuiwa. Kinachozuiwa ni vi-plastic hivi transparent ambavyo huwa vinafungia karanga, ubuyu etc visitumike kuendea sokoni/dukani kubebea bidhaa. Hakuna mtu atakamatwa kwa kuuza karanga kwenye kifungashio cha plastiki” ameeleza waziri Makamba katika mtandao wa Twitter kuwaeleza wananchi.

Hata hivyo, Makamba ameeleza kuwa zipo bidhaa ambazo lazima zifungwe kwenye mifuko ya Plastiki ili kulinda ubora wa bidhaa hizo kama magodoro, peremende na biskuti hivyo bidhaa kama hizo zitaendelea kuwa kwenye mfumo huo wa kufungwa kwenye vifungashio vya Plastiki.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post