NAIBU SPIKA GUAIDO AKAMATWA


Maafisa wa upelelezi wa Venezuela wamemkamata kiongozi wa ngazi ya juu wa bunge linalotawaliwa na upinzani, Edgar Zambrano, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni dhidi ya wabunge walioamua kujiunga na vuguvugu lililoshindikana na kumuondoa madarakani Rais Nicolas Maduro mwezi uliopita. 

Zambrano ni naibu wa spika wa Juan Guaido, mtu anayetambuliwa kama kiongozi wa mpito wa Venezuela na mataifa zaidi ya 50, na ambaye aliongoza vuguvugu la kumuondoa madarakani Maduro mnamo Aprili 30. 

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani hatua hiyo ya kukamatwa kwa Edgar Zambrano. "Kinachotokea nchini Venezuela ni aibu .. Watu wanakufa, hawana chakula, hakuna maji. Hii ni moja ya nchi zilizo tajiri sana ulimwenguni. Na sasa wanaishi vibaya sana. 

"Na tunafanya kazi kwa bidii juu ya tatizo hilo na tunajitahidi kuwa wagumu," amesema Rais Donald Trump. 

Kwa upande mwingine, Mahakama Kuu ya Venezuela iliwashtaki wabunge watatu kuunga mkono uasi wa Guaido uliosababisha siku mbili za mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527