SERIKALI KUWA NA MCHAKATO WA KUAJIRI WATAALAM WA LISHE KILA KIJIJI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo  jambo ambalo hupelekea  udumavu   kwa watoto ,kwa kusababishwa na lishe duni,Serikali ina mchakato wa kuajiri wataalam wa lishe wawili  kwa kila kijiji hapa nchini hali  itakayosaidia kutoa elimu ya lishe  kwa kila kaya.

Hayo yamesemwa  Mei 7,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii ,jinsia Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa     Viti Maalum  Zainab Mwamindi aliyehoji mpango mkakati wa serikali wa kuajili wataalam wa lishe katika vijiji.

Akijibu swali hilo,Mhe.Ndugulile alisema wizara ya Afya ,Mandeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto pamoja na Wizara ya Ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na serikali za mitaa,TAMISEMI zina mchakato wa kuajiri wataalam wa lishe wawili wawili kwa kila kijiji kwa ajili ya kutoa elimu umuhimu wa lishe bora.

Hata hivyo,Mhe.Ndugulile amesema serikali inaendelea kupambana na utapiamlo pamoja  na lishe iliyopitiliza ambapo asilimia 10 ya     Watanzania wanavitambi.

Vipaumbele vya serikali vinavyolenga kupunguza utapiamlo  ifikapo mwaka 2021  ni pamoja na kupunguza viwango vya udumavu  chini ya umri wa miaka mitano  kutoka asilimia 34% mwaka 2015  hadi 28% ,kudhibiti viwango vya ukondefu  kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano  ibaki chini ya 5% kama ilivyo sasa,Kupunguza viwango vya watoto  wanaozaliwa na uzito pungufu  kutoka 7%  kwa mwaka 2015 hadi 5%.

Vipaumbele vingine ni kupunguza idadi ya wanawake walio katika umri wa uzazi  miaka 15 hadi 49  wenye upungufu wa damu  kutoka 44.7% kwa mwaka 2015 hadi kufikia 33%,kupunguza tatizo la upungufu wa vitamin A Kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miezi 59 kutoka 33% hadi kufikia 26% na kupunguza uzito uliozidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kubaki asilimia 5%.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post