TFDA KANDA YA KATI YASEMA ITAENDELEA KUKAGUA NA KUDHIBITI VIPODOZI FEKI NA VILIVYOISHA MUDA

Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma.

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA   imesema itaendelea   kukagua na kudhibiti bidhaa za vipodozi na bidhaa nyingine na kuhakikisha bidhaa ambazo zinamfikia mwananchi zinakuwa  zenye ubora ,salama na fanisi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati inayo simamia mikoa ya Dodoma,singida pamoja na morogoro na Halmashauri zake zote Benedict Blush amesema  TFDA  imepewa jukukumu la kuthibiti,ubora,usalama pamoja na ufanisi wa bidhaa za chakula  dawa,vipodozi,vifaa tiba pamoja na vitendanishi.

Aidha amesema mamlaka hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya chakula na dawa No 1 sura ya 219 huku akizungumzia mifumo ya udhibiti ambayo mamlaka ya chakula na dawa  imekuwa ikitumia katika bidhaa za vipodozi na bidhaa nyingine.

Mbali na hilo pia amezungumzia  vipodozi vyenye viambato  vya sumu kama zebaki hii imekuwa na tabia ya kupenya kwenye ngozi na kadri  inavyo endelea kurundikana katika  mwili  kunaweza kuleta shida ya ini.

Katika hatua nyingine amesema kwa wale ambao wamekuwa wakitumia viambato hivyo inaweza kusababisha kansa ya damu na hatimae kupelekea  kupoteza maisha huku akigusia kwa upande wa wakina mama wajawazito ambao wamekuwa na tabia ya kutumia vipodozi kipindi cha ujazito.

Hata hivyo, amesema kama serikali inaendelea kuweka mkazo katika uthibiti wa vipodozi ili kuondoa madhara kama ambayo yanaweza kuajitokeza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527