Friday, April 12, 2019

SUGU AMUOMBA RAIS MAGUFULI AONGEZE MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI

  Malunde       Friday, April 12, 2019

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi  maarufu kama ‘Sugu’ amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akienda Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani asisahau kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma kwa sababu miaka yake minne hajawahi kuongeza hata kidogo.


Sugu ametoa kauli hiyo wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwa nidhamu kubwa anamuomba Rais atakapokuwa Mbeya atangaze ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi kwa sababu, tangu aingie madarakani na huu ni mwaka wa nne mishahara haijaongezeka.

“Wafanyakazi wana hali mbaya sana maeneo yote ya nchi hii. Pia, aangalie suala la wastaafu wapo wengi wengine ni mwaka wa pili sasa hawajalipwa mafao yao,” amesema Sugu

“Katika idara mbalimbali ikiwamo za ulinzi na usalama kama magereza, polisi ni miaka miwili sasa wastaafu wapo katika kota hawana nauli za kubebea mizigo kurudi kwao.”

Amewaomba Mawaziri kama suala la nyongeza ya mishahara halipo mezani warudi na kuangalia upya ili Rais atakapokwenda Mbeya atangaze ongezeko kwa watumishi wa umma, ili kuwezesha kupata nafuu ya maisha.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post