KIMBUNGA ADA CHAUA WATU 65 ZIMBABWESehemu ya Eneo lililoathiriwa na Kimbunga.

Watu 65 wamefariki dunia mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga kiitwacho Ida.

Kati ya watu waliopoteza maisha ni katika shule mbili ambapo tufani hiyo iliwakumba usiku wa manane wakiwa wamelala. Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu wa miundo mbinu katika jimbo la Manicaland karibu na mpaka wa Zimbabwe na Msumbiji.

Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani waliko, hali inayohofiwa kwamba huenda inaweza ongeza idadi ya waliopoteza maisha.

Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake Mashariki ya Kati na kurejea nchini mwake kutokana na janga hili. Hata hivyo, kasi ya kimbunga hicho inapungua japo kuwa tayari kimesababisha madhara makubwa huku takribani watu 200 wakiwa hawajulikani walipo.

Nchini Msumbiji na Malawi kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 120. Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho kilichoyakumba maeneo hayo kikiwa na mwendo wa kasi wa kilomita 177 kwa saa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post