NASSARI AMPONZA MBUNGE MWINGINE WA CHADEMA

Spika wa Bunge anafikiria hatua za kinidhamu za kumchukulia Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijualikali kufuatia kauli za kejeli dhidi ya Bunge.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba kauli hizo zimetolewa na Mbunge huyo siku ya jana, Machi 17, wakati akizungumza na wanahabari katika mkutano wa Joshua Nassari ambaye amevuliwa Ubunge wiki iliyopita.

Katika mkutano huo, Lijualikali alishangazwa na kitendo cha Spika kumvua ubunge Nassari wakati Mbunge huyo alipodai kuwa alitimiza wajibu wake wa kulitaarifu bunge juu ya matatizo anayopitia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post