FILAMU YA LAANA YA MKE YATWAA TUZO YA HESHIMA

Filamu ya Lana ya Mke
Mwandaaji wa Filamu Bryton kutoka Mwanza akiwa na tuzo ya heshima ya filamu bora Kanda ya ziwa yenye maudhui ya kitaifa Februari 23,2019 usiku wa tuzo za SZIFF .


Filamu ya Laana ya Mke iliyoigizwa na wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kushinda Tuzo ya Heshima Filamu Bora yenye maudhui ya kitaifa Kanda ya Ziwa.

Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga, Ibrahim Juma Songoro maarufu 'Songoro Gadafi' amesema hakuamini kama Azam Tv Sinema Zetu ingewapa tuzo hiyo.

"Siamini Kama Azam Tv Sinema zetu imetutunukia tuzo hiyo,kwani tulikata tamaa baada ya kutolewa katika fainali za SZIFF, hatukuwa na wazo kama tutapewa heshima hii",alisema Gadafi.

"Naomba watanzan kuendelea kutuunga mkono katika kazi zetu kwani tunajitahidi kuigiza maisha halisi ambayo huwa yanatoa ujumbe mzuri katika jamii,nasi tutaendelea kutoa kazi nzuri zenye kiwango cha kitaifa na kimataifa",aliongeza Gadafi.

Filamu ya "Laana ya Mke" ilizinduliwa rasmi usiku wa Machi 23 kuamkia Machi 24,2018 mjini Shinyanga na kuhudhuria na wapenzi wa filamu ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga akiwemo Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo.

Filamu hiyo inahusu majanga na laana wanazopata wanaume wababe,wasio na fadhila wanaotafuta mali na wake zao kisha kuwafanyia ukatili.

Miongoni mwa wasanii walioshiriki katika Filamu hii iliyoongozwa na Director mahiri Dave Skerah yumo Blandina Chagula ‘Johari’, Ibrahim Songoro‘Songoro Gadafi’,Magreth Emmanuel, Mariam Bilal, Najma Shahel,Edward Joseph na Mzee Salum Kawelewele.

TAZAMA HAPA SEHEMU YA FILAMU YA LAANA YA MKE

Filamu ya Laana ya Mke  ipo Sokoni /mtaani,pata nakala yako sasa,piga simu namba 0767831036 ,0712686129 au 0743184350 itakufikia popote ulipo.

ANGALIA PICHA <<HAPA>> WAKATI WA UZINDUZI WA FILAMU YA LAANA YA MKE

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post