Saturday, March 24, 2018

Picha : SHUHUDIA HAPA UZINDUZI WA FILAMU YA 'LAANA YA MKE' - BONGO MOVIES SHINYANGA...MAMBO NI MOTOOOO!!

  Malunde       Saturday, March 24, 2018

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akionesha Filamu ya Laana ya Mke baada ya kuizindua katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga Machi 23,2018Hatimaye Filamu ya "Laana ya Mke" imezinduliwa rasmi usiku wa Machi 23 kuamkia Machi 24,2018 katika ukumbi wa katika ukumbi wa NSSF ya zamani “CCM mkoa wa Shinyanga" na kuhudhuria na wapenzi wa filamu ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro.

Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo pamoja na mwigizaji maarufu wa Filamu Blandina Chagula 'Johari' ambaye kwao ni Shinyanga pia amejitolea kushiriki katika filamu hiyo ya "Laana ya Mke".

Akizindua Filamu hiyo,Matiro aliwapongeza wasanii mkoani Shinyanga kwa kutoa filamu hiyo nzuri inayotoa mafundisho katika jamii  ambayo itasaidia kuhakikisha kila mmoja anamheshimu mwanamke.

"Hii ni filamu nzuri,naomba muendelee kutoa elimu kwa kuangalia hali halisi ya mazingira yanayozunguka,sisi serikali tunatambua kazi nzuri mnayofanya katika kuielimisha jamii",alisema.

"Filamu hii inaendelea kuutangaza mkoa wa Shinyanga na tunaamini kupitia Bongo Movies Shinyanga tutapata wasanii wengine watakaoigiza katika kiwango cha kimataifa kama alivyofanya Stephen Kanumba na Johari ambao kwao ni Shinyanga",alieleza Matiro.

Miongoni mwa wasanii walioshiriki katika Filamu hii iliyoongozwa na Director mahiri Dave Skerah yumo  Blandina Chagula ‘Johari’, Ibrahim Songoro‘Songoro Gadafi’,Magreth Emmanuel, Mariam Bilal, Najma Shahel,Edward Joseph na Mzee Salum Kawelewele.

Filamu hiyo inahusu majanga na laana wanazopata wanaume wababe,wasio na fadhila wanaotafuta mali na wake zao kisha kuwafanyia ukatili.

Tayari Filamu ya Laana ya Mke  ipo Sokoni /mtaani,pata nakala yako sasa,piga simu namba 0767831036 ,0712686129 au 0743184350 itakufikia popote ulipo.

Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke,ametusogezea picha 52 za matukio yaliyojiri tazama hapa chini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kuzindua Filamu ya Laana ya Mke.Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Ibrahim Juma Songoro.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizindua Filamu ya Laana ya Mke.Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Ibrahim Juma Songoro (aliyevaa shati jeupe).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akionesha Filamu ya Laana ya Mke baada ya kuizindua.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akionesha Filamu ya Laana ya Mke.

Tunashuhudia uzinduzi.....
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akiangalia kava ya CD ya Filamu ya Laana ya Mke.
Meza kuu wakiangalia Filamu ya Laana ya Mke

Wapenzi wa Filamu wakiwa ukumbini
Meza kuu

Kulia ni MC Tumaini akifurahia jambo na wadau wa Filamu

Wadau wakiwa ukumbini
Blandina Chagula 'Johari' akiwa na wapenzi wa filamu kushuhudia uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwataka wasanii wa uigizaji kutoendekeza migogoro

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Ibrahim Songoro akielezea kuhusu Filamu ya Laana ya Mke
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na Director wa Filamu ya Laana ya Mke, Dave Skerah

Blandina Chagula 'Johari' akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke, ambapo alisema amejitolea kwa gharama zake mwenyewe kuigiza katika Filamu ya Laana ya Mke baada ya kufurahishwa na wasanii wa nyumbani/Shinyanga.Aliwataka wasanii kutoogopa kumshirikisha katika kazi zao

Wadau wakiwa ukumbini
Afisa Utamaduni mkoa wa Shinyanga Mariam Ally akitambulisha wageni mbalimbali ukumbini
Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fissoo akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu ya Laana ya Mke

Waigizaji katika Filamu ya Laana ya Mke. Kulia ni Mariam Bilal akisoma risala kuhusu Bongo Movies Shinyanga
Waigizaji katika Filamu ya Laana ya Mke wakijiandaa kuanza Kuuza/kusambaza CD za filamu hiyo ukumbini
Mwigizaji Magreth Emmanuel akimwambia jambo Songoro Gaddafi wakati wa kuuza CD ukumbini

Mkurugezi wa Malunde1 blog,akiwa ameshikilia CD ya Filamu ya Laana ya Mke.
Johari akifurahia jambo baada ya kununua CD ya filamu ya Laana ya Mke
Johari akiteta jambo na Songoro Gaddafi
Kundi la Muziki 'Nyumbu Wajanja' wakitoa burudani
Wadau wakiwa ukumbini


Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Ibrahim Songoro akiwashukuru wadau mbalimbali ikiwemo kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa kushiriki kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha uzinduzi wa Filamu ya Laana ya Mke.Johari akiwa na Director wa Filamu ya Laana ya Mke, Dave Skerah 
Waandishi wa habari wakimfanyia mahojiano Johari 

Picha zote kwa hisani ya Kadama Malunde - Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post