MTOTO ANAYEDAIWA KUFUNGIWA KABATINI HATOI SAUTI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, January 4, 2019

MTOTO ANAYEDAIWA KUFUNGIWA KABATINI HATOI SAUTI

  Kanyefu       Friday, January 4, 2019

 Wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi wa hali ya mtoto anayedaiwa kufungiwa kabatini kwa miezi mitano, madaktari wametaja tatizo jingine walilolibaini kwa mtoto huyo kuwa hatoi sauti.

Mtoto huyo aliyelazwa wodi ya watoto wenye utapiamlo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, amegundulika kuwa na tatizo la kutotoa sauti hata anapolia, hivyo kuwafanya madaktari kuanza kutafuta sababu.

Akizungumza na Mwananchi hospitalini hapo jana, Ofisa Muuguzi, Dina Msesa alisema hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika baada ya kumwanzishia lishe ya vyakula vya kuboresha afya yake, lakini tatizo lipo kwenye utoaji wa sauti.

“Mtoto huyu hatoi sauti yoyote wala halii, ila ametulia jambo linalofanya wataalamu waanze kukuna vichwa kutafuta tatizo,” alisema Msesa.

Kuhusu mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mtumishi wa ndani, alisema afya yake imeimarika na mkono uliokuwa umeumia umepona ambapo sasa anaweza kuunyayua tofauti na awali.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post