Wednesday, January 9, 2019

MC PILIPILI ATUHUMIWA KUCHUMBIA MPENZI WA KIDUME KINGINE

  Malunde       Wednesday, January 9, 2019

Mchekeshaji maarufu bongo, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' ambaye hivi karibuni amemvisha pete mchumba wake, amefunguka juu ya tuhuma zinazodaiwa kuwa ametumia pesa kumpata mwanamke huyo kutoka kwa mwanaume wake wa zamani.

Akizungumza na www.eatv.tv, MC Pilipili amesema kwamba anamuhurumia kijana huyo, lakini anaamini atapata mwanamke mwengine kwani wanawake ni wengi Tanzania.

“Aisee nampa pole, Tanzania inaonesha wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwa hiyo sio rahisi kwa yeye kutembea na mwanaume mwingine, lakini ni rahisi kupata mwanamke, atapata mwanamke mwingine, kwani wanawake ni wengi Tanzania na duniani”, amesema Mc Pilipili.

Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita, Mc Pilipili amechumbia msichana mmoja anayejulikana kwa jina la Philomena Thadey maarufu kama 'Cute Mena', na baada ya muda mfupi zikaibuka tuhuma mitandaoni kuwa alikuwa mchumba wa mwanaume mwingine hapo kabla.
Chanzo- EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post