SHILOLE AWACHANA 'WADANGAJI' WANAONYEMELEA NDOA YAKE


Shilole akiwa na mume wake, Uchebe.

Mwanamuziki Shilole amewataka wadada wa mjini 'wadangaji' kukoma kumfuatilia mume wake ' Uchebe' kwa madai kwamba anamtunza na kumpendezesha.

Shilole amesema hayo baada ya kugundua kwamba wapo manyamera wanaonyemelea penzi la mume wake ambapo akidai kwamba zamani wakati akiwa hana kitu hawakuonekana kumfuata.

"Niliridhika na hali yako tangu mwanzo mpaka sasa una'shine' ila wadangaji msivyo na haya mnaanza kumwambia mume wangu Uchebe 'amekuwa handsome'", amesema Shilole.

Shilole na Ashraf Uchebe walifunga ndoa Desemba 7, 2017 ambapo awali msanii huyo alipondwa kwa kukubali kufunga ndoa na Uchebe huku maneno yakiwa kwamba hawaendani kiuwezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post