CHADEMA WATAKA KUFANYIKA MABORESHO YA DAFTARI LA WAPIGA KURA MAPEMA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Pwani kimetaka kufanyika kwa maboresho ya daftari la wapiga kura mapema ili kuepuka zima moto.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 24, 2018, Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye amesema kazi hiyo ifanyike kwa muda muafaka na mapema ili baadaye isije kufanyika kwa dharura.

"Ili kulinda haki za raia tunapenda kuikumbusha serikali kuwa ni lazima zoezi la kuhakiki daftari la wapiga kura ifanyike kwa muda muafaka bila kuifanya kama zoezi la dharura ili kila mpiga kura apate haki yake ya kuandikishwa",amesema Sumaye.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa tume huru ya Uchaguzi, Sumaye amesema; "Kwa ajili ya mapungufu kwenye muundo mzima wa Tume ya uchaguzi,kama jambo la umuhimu wa kipekee Tume HURU ya uchaguzi ambayo haitapewa maelekezo na utawala na itakuwa na watumishi wake bila kutegemea watumishi wa serikali,iundwe haraka kwa vyovyote kabla ya uchaguzi ujao"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post